Articles

Affichage des articles associés au libellé Roma

Baba Mtakatifu Francis asema Mashahidi wa Ufufuko wa Yesu Walikuwa Wanawake

Image
Baba Mtakatifu Francisko, katika Katekesi yake ya Jumatano 3 Aprili alisema kwamba, Ufufuko wa Kristo ni kiini cha imani ya Kanisa, msingi wa matumaini ya utekelezaji wa ahadi za Mungu pamoja na ushindi dhidi ya dhambi na mauti. Akifanunua kanuni ya Imani katika mafundisho yake ya kila Jumatano, Baba Mtakatifu alisema, Mashahidi wa kwanza wa ufufuko wa Kristo walikuwa ni wanawake; waliosukumwa na upendo kwa Kristo kiasi kwamba, wakajihimu kwenda kaburini, huko wakapewa Habari Njema ya Ufufuko waliyowashirikisha Mitume.   Baba Mtakatifu Francis akihutubia mahojaji katika viwanja vya Mt Petro, Roma