Baba Mtakatifu
Francisko, katika Katekesi yake ya Jumatano 3 Aprili alisema kwamba, Ufufuko wa
Kristo ni kiini cha imani ya Kanisa, msingi wa matumaini ya utekelezaji wa
ahadi za Mungu pamoja na ushindi dhidi ya dhambi na mauti. Akifanunua kanuni ya
Imani katika mafundisho yake ya kila Jumatano, Baba Mtakatifu alisema,
Mashahidi wa kwanza wa ufufuko wa Kristo walikuwa ni wanawake; waliosukumwa na
upendo kwa Kristo kiasi kwamba, wakajihimu kwenda kaburini, huko wakapewa
Habari Njema ya Ufufuko waliyowashirikisha Mitume.
|
Baba Mtakatifu Francis akihutubia mahojaji katika viwanja vya Mt Petro, Roma |
Baba Mtakatifu anasema, hii ni changamoto kwa
waamini kuweza kushirikisha ile furaha inayopata chimbuko lake kutoka kwa
Kristo Mfufuka. Katika historia ya maisha na utume wa Kanisa, wanawake wamekuwa
wepesi kuwafungulia wengine mlango wa imani kwa Kristo, kwani imani ni jibu
makini la upendo.
|
Maelfu ya watu walifurika kumsikiliza Baba Mtakatifu |
Kwa njia ya jicho la imani, waamini pia wanayo
bahati ya kukutana na Yesu Kristo Mfufuka na kuonja uwapo wake: katika Maandiko
Matakatifu, Ekaristi Takatifu na Sakramenti mbali mbali za Kanisa; matendo ya
huruma, wema na msamaha ni matukio ambayo yanaonesha uwapo endelevu wa Kristo
katika hija ya maisha ya wafuasi wake hapa duniani.
|
Umati ukifuatilia mafundisho ya katekesi ya Papa kila Jumatano |
Baba Mtakatifu Francisko anahitimisha Katekesi
yake kwa kuwataka waamini, mahujaji na watu wenye mapenzi mema kuimarisha imani
yao kwa Kristo Mfufuka ili waweze kuwa kweli ni alama wazi ya ukuu wa maisha na
matumaini dhidi ya ubaya, dhambi na kifo.
|
Baba Mtakatifu akisalimiana na umati uliofika katika Viwanja vya Vatican |
|
Wakubwa kwa wadogo walifurika kumsalimia Baba Mtakatifu |
Source: www.radiovaticana.va
Commentaires