Articles

Affichage des articles associés au libellé utalii

Tanzania Yashiriki Katika Maonyesho Ya Kimataifa ya Utalii Paris

Image
Tanzania kupitia Bodi ya Utalii Tanzania ilishiriki katika maonyesho ya Kimataifa ya Utalii yaliyofanyika mjini Paris, Ufaransa kuanzia Machi 21 na kuhitimishwa Jumapili Machi 24, 2013. Katika banda la Tanzania, Bi Gloria Munhambo, Ofisa Mkuu wa Maelezo ya Utalii na Ofisa Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Kanda ya Mwanza, akiongozana na maofisa wengine wa Bodi ya Utalii na Mamlaka ya Hifadhi za Wanyapori Tanzania (TANAPA) walikuwa na kazi kubwa ya kutangaza vivutio mbali mbali vya Tanzania kwa wageni waliotembelea banda la Tanzania.