TANZIA: PADRE MICHAEL MASSAWE CSSp

Jumuiya ya Wamisionari na Watawa wa Shirika la Roho Mtakatifu wanasikitika kutangaza kifo cha mwanashirika mwenzao Padre Michael Massawe CSSp kilichotokea jumatatu tarehe 26 Octoba 2015 katika mji wa La Croix Valmer nchini Ufaransa. Maziko Maziko yatafanyika Ufaransa Ijumaa Novemba 6 saa nane na nusu mchana (saa za Paris sawa na saa kumi na nusu saa za Afrika Mashariki). Kwa desturi za wamisionari wa Roho Mtakatifu maziko hufanyika mahali alipofia. Historia fupi Padre Michael Massawe alizaliwa Septemba 29 mwaka 1960 katika kijiji cha Keni wilayani Rombo (Kilimanjaro). Aliweka nadhiri za kitawa Julai 6, 1988 katika novisia ya Magamba, Lushoto (Tanga). Alipewa daraja la Upadre tarehe 28 mwezi mei 1993 Usa River mjini Arusha.