Kilimo: Ajira Mbadala Kwa Vijana Tanzania

Nchini Tanzania inakadiriwa kuwa zaidi ya vijana 900 000 wanaingia kwenye soko la ajira kila mwaka. Hata hivyo ni ajira 50 000 hadi 60 000 tu mpya zinazopatikana kwa mwaka hivyo kuwaacha vijana wengi wakiwa hawana kazi. Kutokana na wimbi la ukosefu wa ajira, mishahara midogo kwa wale wenye ajira rasmi, baadhi ya vijana wameamua kuwekeza kwenye kilimo kama njia mbadala ya uzalishaji mali.

Mike Utouh na Roman Massawe ni baadhi ya vijana walioamua kuwa wakulima wa vitunguu wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro ili kujipatia mapato mbadala.



Kilimo: Ajira Mbadala kwa Vijana by Simplisphoto

Je elimu inayotolewa nchini Tanzania inamsaidiaje kijana kuweza kujitegemea au kuwa na ujuzi unaohitajika na waajiri? Je ni kwa kiwango gani elimu itolewayo Tanzania katika ngazi ya sekondari na vyuo inamsaidia kijana kuweza kuwa mjasiriamali ili kutengeneza ajira mpya badala ya kusubiriwa kuajiriwa?

Commentaires

Posts les plus consultés de ce blog