TANZIA: MAMA EMMY SHIRIMA AFARIKI DUNIA MJINI PARIS

Tunasikitika kutangaza kifo cha Mama Emmy S. Shirima kilichotokea Mei mosi mjini Paris katika Hospitali ya Hôpital Européen Georges Pompidou mjini Paris. 

Mama Shirima alikuwa mfanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania mjini Paris tangu mwaka 2006. Mama Shirima alikuwa mgonjwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Mwili wa marehemu utasafirishwa kwa ndege kwenda Dar es Salaam, Tanzania Alhamisi Mei 7. Baada ya mwili kufika Dar es Salaam siku ya Ijumaa, ibada ya mazishi itafanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi Sinza Jumamosi Mei 9 saa 7 machana.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nje ya Hospitali 'Hôpital Européen Georges Pompidou', Paris
Ubalozi wa Tanzania mjini Paris ukishirikiana na Watanzania waishio Ufaransa walifanya ibada ya kuuaga mwili wa Mama Shirima leo jioni katika Hospitali ya Georges Pompidou, Paris. Ibada hiyo ilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania, wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania, na wawakilishi kutoka balozi za Kenya, Uganda, Namibia, Msumbiji, Namibia, Zimbabwe na Cape Verde.

 
Picha ya pamoja ya baadhi ya walioshiriki katika ibada ya kumwaga Mama Shirima, Paris

Commentaires

Posts les plus consultés de ce blog