Je Wakifahamu Tumaini Bakery, Kiwanda cha Mikate Rombo?

Kwa miaka mingi ilikuwa desturi kununua mikate Moshi au Himo pindi watu wanapoenda Rombo kwa likizo au kusalimu ndugu jamaa na marafiki. Kwa sasa waweza kusahau kabisa bugudha ya kusafiri na mizigo na mikate kwani mikate na bidhaa nyingine zinapatikana Rombo. Bidhaa safi na bora zinatengenezwa ndani ya wilaya ya Rombo.

Mkate ulio tayari kuuzwa

Mikate iliyo tayari kuwekwa kwenye mifuko ili kuuzwa
Onja Tumaini Bread na bidhaa nyingine maarufu kutoka Tumaini Bakery kiwanda kilichopo Mkuu, Rombo. Tumaini Bakery ipo Mkuu Mjini karibu na Hospitali ya Huruma.
Sr Mary Lauda (kushoto) na mwokaji wa mikate (kulia)



Mikate ikiwa tayari kuingia kwenye tanuru ili kuokwa

Bidhaa zilizo tayari!!!
Tumaini Bakery ni mradi ulioanzishwa na Tumaini Centre kituo kinachoendeshwa na Sr Mary Lauda CDNK ili kupata fedha za kusaidia watoto yatima na walio katika mazingira magumu. Kwa kununua bidhaa za Tumaini Bakery unawekeza katika maisha ya watoto wengi yatima au wanaoshi katika mazingira magumu katika wilaya ya Rombo.
Mikate, keki, na biskuti ni baadhi ya bidhaa za Tumaini Bakery

Gari likipeleka mikate kwenye soko
Kutokana na uchanga wa mradi huu, zipo changamoto mbalimbali zinazokabili mradi huu zikiwapo ukosefu wa mtaji, soko, umeme wa uhakika, ugumu wa kuingia kwenye soko kwani tayari zipo bidhaa nyingine kwenye soko na ukosefu wa watu wenye fani ya uokaji wa mikate na bidhaa za mikate.

Commentaires

Posts les plus consultés de ce blog

Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2023 Wilaya ya Rombo

WHAT DAR ES SALAAM BUS RAPID TRANSIT WILL LOOK LIKE!